Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limewakashifu baadhi ya maafisa wa usalama kanda ya pwani ambao wanadaiwa kuwapiga wenyeji kiholela kwa misingi ya kufanikisha amri ya kutotoka nje nyakati za usiku.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid ameyataja mauaji ya kijana mmoja mwenye umri wa miaka 23 eneo la Ukunda ambaye alifariki tarehe mosi mwezi huu wa Aprili kama ya kinyama.
Amezitaka asasi husika kuwachukulia hatua maafisa wa usalama waliohusika na mauaji hayo.