Liverpool haikamatiki, asema Kocha Jurgen Klopp baada ya kipigo cha Watford

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake itafufuka tena baada ya ushindi wa kushangaza dhidi ya Watford katika mechi yao ya mwisho ya Ligi Kuu.

Vijana wa Klopp ambao hawajawahi kupata kichapo tangu kuanza kwa msimu huu, walicharazwa magoli 3-0 na Watford ambayo inajizitatiti kutoondolewa katika Ligi hiyo.

Kichapo hicho kina maana kuwa Liverpool hawatamaliza msimu huu bila kufungwa, rekodi ambayo inaendelea kushikiliwa na Arsenal chini ya kocha Arsene Wenger.

Tangu Mfaransa huyo kukamilisha msimu wa mwaka 2003/04 wa Ligi Kuu bila kichapo, hakuna timu nyingine ya Uingereza iliyovunja rekodi hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.