Ligi kuu Uingereza, Arsenal yaibutua Newcastle

Ligi kuu ya Uingereza imeendelea jana usiku kwa mchezo mmoja tu kupigwa kwenye uwanja wa Emirates, ambapo washika bunduki wa London Arsenal ilipokutana na NewCastle United.

Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa, Arsenal waliibuka na ushindi wa bao 2-0. Mabao yaliyofungwa na Aaron Ramsey na Alexandre Lacazette yamewawezesha washika bunduki hao kupaa hadi nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ya EPL.

Leo itakuwa ni siku ya Manchester United kukwea hadi nafasi ya tatu iwapo watailima Wolverhampton Wanderers saa nne kasorobo saa za Afrika Mashariki na kutoka na pointi tatu. Hata hivyo Fulham watakuwa ugenini dhidi ya Watford.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.