Kwa mujibu wa Naville, ambaye aliwahi kucheza na Ole Gunnar, ni kwamba kuna mbinu fiche ya kumng’oa Solskjaer klabuni Manchester United. Raia huyo wa Uingereza amesistiza kwamba kutemwa nje kwa Mashetani wekundu katika hatua ya makundi sio pigo la kustaajabisha.
Hata hivyo, ilisalia ndoto huku Leipzig, ambao walishiriki nusu fainali msimu uliopita wakisukwa upya na kufuzu kwa kuwazima Mashetani Wekundu.
Miamba hao wa Bundesliga walianza mechi hiyo ya Kundi H kwa matao ya juu, huku Angeliño akifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya pili ya mchezo, kombora lake likimshinda maarifa David de Gea.
Amadou Haidara alisawazisha bao hilo dakika kumi baadaye akimalizia vyema krosi ya Angeliño.
Wenyeji walidhania kuwa walipiga msumari wa mwisho kwenye mchezo huo lakini teknolojia ya VAR ilifuta bao la Orban. United walirejea mchezoni baadaye lakini walishindwa kuonja wavu licha ya kutawala dakika 15 za mwisho za awamu ya kwanza.
Justin Kluivert, alitoka benchi na kubadilisha matokeo kuwa 3-0 kunako dakika ya 69 kabla ya Bruno Fernandes kufungia United bao la kwanza kupitia mkwaju wa penalti.
Klabu ya Ligi Kuu iliendelea kukaza kamba huku juhudi zao zikizaa matunda katika dakika ya 83 wakati Pogba alifunga bao la pili akitumia kichwa kupachika mpira wavuni baada ya mpira kumgonga Harry Maguire.
Jaribio la mwisho la United liligonga mwamba huku wenyeji wakishikilia ushindi wao. Vijana wa Ole Gunnar Solskjaer wamebanduliwa kwenye Champions League na sasa wanajiunga na Arsenal na Tottenham Hotspur katika mkondo wa pili wa mashindano hayo.
Ninawaombea Hao Man_useless Taji Hilo La Europa League