Klabu zote za EPL zinafaa kufaidi mgao wa Ksh 20M, asema kocha wa Bandari

Mkufunzi wa klabu ya Bandari Ken Odhiambo ameitaka wizara ya michezo nchini kuhakikisha klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu nchini KPL zinanufaika na mpango wa serikali kuu wa kuwapamba wachezaji na Kshs 10, 000 kila mchezaji kila mwezi kipindi hiki cha janga la virusi vya Covid-19.

Hii inakuja baada ya baadhi ya klabu kudaiwa kupigwa nje ya mpango huo. Klabu ya Tusker FC, Ulinzi Stars, Bandari FC, KCB, Wazito, Western Stima na Poster Rangers ni miongoni mwa klabu zinazodaiwa kukosekana kwenye orodha ya vilabu vitakavyofaidi mradi huo wa serikali.

Waziri wa michezo nchini Balozi Amina Mohammed alitangaza kwamba wachezaji kumi na wawili wa vilabu vya KPL na viongozi wao watano watapigwa jeki kwa kupewa Kshs 10, 000 kila mwezi kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali.

Odhiambo aidha amekanusha madai kwamba klabu ya Bandari inapunguza idadi ya wachezaji wake kutoka 30 hadi 25.

”Hizo ni rumours tu wala hakuna kitu kama hicho. Tumesimamisha kila shughuli kipindi hiki cha Corona na tunasubiri Juni 6 kama tutapewa go-ahead ya kurudi kiwanjani,’ amesema Odhiambo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.