Kilifi | Mwanafunzi wa kidato cha kwanza ajitoa uhai

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya upili ya Franz Joseph Kaunti ya Kwale amepatikana amejinyonga nyumbani kwao Mtwapa Kaunti ya Kilifi.

Hilda Kimanthi mwenye umri wa miaka 15 amejitoa uhai wake baada ya kupewa likizo ya lazima kwa kupigana na mwanafunzi mwingine.

Kulingana na shangaziye ni kwamba baada ya kufukuzwa shule Hilda alimweleza babake ambaye alimrudisha shuleni mapema wiki hii ili kusuluhisha lakini walipofika wakatakiwa kurudi nyumbani hadi hapo jana Alhamisi, jambo ambalo lilimpa Hilda mawazo mengi hadi kufikia maamuzi ya kujitoa uhai wake.

Aidha, Kamanda wa polisi katika Kaunti ndogo ya Kilifi Kaskazini, Esau Ochorokodi amesema wanaamini kwamba msichana huyo alijitoa uhai kwasababu ya mawazo aliyoyapata baada ya kufukuzwa shule hivyo basi akaziomba shule kutumia njia nzuri wanapokabiliana na visa vya utovu wa nidhamu mashuleni.

Wakati uo huo ameongeza kua wanafanya uchunguzi zaidi ili kubaini iwapo kuna sababu nyingine iliyosababisha Hilda kujitoa uhai.
Mwili wake umepelekwa katika Hifadhi ya Hospitali ya Mkoa wa Pwani huku familia ikiendelea na mipango ya mazishi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.