Kibibi Ali awataka wenyeji wa Kilifi kuzingatia tahadhari kuhusu maambukizi ya virusi vya Corona

Wakaazi wa kaunti ya kilifi wamehimizwa kutilia maanani maagizo ya serikali ya kujikinga dhidi ya virusi vya korona.
Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirika la kutetea haki za kina mama la Kilifi mums, Kibibi Ali ambaye amesema kuwa tayari visa vya virusi hivyo vimeripotiwa baada ya naibu gavana wa Kilifi Gideon Saburi kupatikana na virusi hivyo.
Mwenyekiti huyo ameonekana kugadhabishwa na hatua ya serikali kufunga biashara za masoko ya chakula katika kaunti ya Kilifi jambo ambalo limeibua hisia mbali mbali kwa wenyeji.
Aidha Kibibi ameitaka serikali kutafuta njia mbadala ili kuzuia uwezekamo wa kushuhudiwa kwa baa la njaa katika kaunti ya Kilifi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.