KHALWALE NA MUTHAMA WAPINGA SHUGHULI ZA KUKUSANYA SAINI ZA KUUNGA MKONO BBI

Mchakato wa kuirekebisha katiba kupitia ripoti ya BBI unapoendelea kushika kasi nchini baadhi ya viongozi ambao wanaegemea upande wa naibu wa rais Daktari William Samoei Ruto wamepinga vikali shughuli za kukusanya saini za kuunga mkono mchakato huo.
Akihutubu huko Mvindeni kaunti ya Kwale aliyekuwa Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale amesema kwamba huenda ripoti hiyo ikazifaidisha jamii chache nchini tofauti na inavyodhaniwa kuwafaidi wakenya.
Wakati uo huo aliyekuwa Seneta wa Machakos Johnstone Muthama amepinga ripoti hiyo na kusema haijajumuisha makabila yote nchini katika mfumo mpya wa serikali huku akitaka ifanyiwe marekebisho kabla ya katiba ya nchi kubadilishwa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.