Kenya yathibitisha visa tisa vipya vya maambukizi ya virusi vya Corona

 

Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema taifa la Kenya limethibitisha visa 9 vipya vya maambukizi ya virusi vya Corana na idadi kufika 25 ambapo miongoni mwa 9 hao 7 ni Wakenya na 2 wakiwa raia wa kigeni.
Wakenya wamelaumiwa kwa madai kwamba wengi wameonyesha utovu wa nidhamu, tabia ambayo ni pigo katika juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona huku watu 3 miongoni mwa wakenya walioambukizwa ni wale ambao walitangamana na wale waliokuwa wameambukizwa hapo awali.
Kagwe amesema kaunti zilizoathirika zaidi ni Nairobi, Mombasa, Kilifi, na Kwale.
Ameongeza kuwa takribani watu 745 wanaendelea kutafutwa kwa kutangamana na walioathirika na kutokana na ongezeko la maambukizi hayo nchini Kagwe amesema leo serikali itatangaza mikakati zaidi ambayo itawekwa ili kuzuia maambukizi zaidi.
Hata hivyo amewataka wamiliki wa hoteli ambako watu wanaorejea nchini wanawekwa karantini kutowatoza ada za juu kipindi hiki na kusema utaratibu wa kuwaweka karantini umeboreshwa na kusema ni habari za kutia moyo kuwa hali za watu walioambukizwa awali virusi vya Corona hali yao inaendelea kuimarika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.