Kenya ‘yamomonyoka’ kwenye viwango vya Fifa

Timu ya taifa ya Kenya almaarufu Harambee Stars imeteremka nafasi mbili hadi nambari 107 katika viwango vipya vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Katika viwango hivyo vya mataifa 211 vilivyotangazwa Julai 25, vijana wa kocha Sebastien Migne, ambao walikuwa wameruka juu nafasi tatu hadi nambari 105 duniani Juni 14, wamepoteza alama sita. Wakenya sasa wana jumla ya alama 1201.

Tanzania ambao walirejea katika AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980, wametupwa chini nafasi sita hadi 137 duniani.

Burundi, ambayo iliingia AFCON kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2019, imeporomoka kwa nafasi 14 hadi nambari 148 duniani.Uganda wamekwamilia kwenye nafasi ya 80 duniani  sudan wakiwa wamepaa nafasi moja 129 nao Rwanda wamepaa nafasi tatu hadi 133.

Ethiopia inasalia katika nafasi ya 150 duniani. Sudan Kusini imeshuka nafasi moja hadi nambari 169 duniani. Djibouti, Somalia na Eritrea ziko katika nafasi tatu za mwisho duniani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.