Kenya U-16 kushiriki mashindano ya Hispania

Timu ya soka ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 16 ya Kenya jana ilipata mwaliko wa kushindana kwenye kombe la Mediterranean International Cup (MIC), na nahodha Teddy Sirma anaona kuwa fursa hii itatimiza matarajio yake ya kucheza klabu ya Ligi ya Premier ya Uingereza (EPL).

Afisa habari wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Ken Okaka amesema timu ya vijana itakwenda Hispania kwa ajili ya maandalizi na kucheza mechi za kirafiki kabla ya kushindana kwenye michuano hiyo itakayofanyika Aprili huko Valencia.

Kenya ilishinda mechi mbili kati ya sita za nje kwenye mashindano ya mwaka jana lakini uchezaji wao ulitosha kwa Sirma kufanya akodolewe macho na Tottenham Hotspur. Vijana hao waliwashinda CF Nevata 6-1, na baadaye kuibanjua 3-0 CE Flaca kwenye kupigiana mikwaju, kabla ya kushindwa na upande wa Marekani Eastern FC, Terres de L’ebre na ASM Belfortaine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.