Kenya | Serikali yaombwa kuajiri watafsiri wa lugha ya ishara katika hospitali za umma

Mkurugenzi mkuu wa shirika ambalo linaangazia maswala ya haki za watoto na wanawake ambao wanaishi na ulemavu la Disability Trust Lizzie Kiama ameitaka wizara ya afya kuajiri watafsiri wa lugha ya ishara kwenye hospitali za hapa nchini.

Kwenye kikao na waandishi wa habari amesema ikiwa serikali itakumbatia hilo basi hatua hiyo itakabiliana na changamoto ambazo watu wenye ulemavu huwa wanazipitia wanapotafuta huduma za matibabu katika hospitali mbali mbali nchini Kenya.

Ametaja walio na ulemavu wa kutoona, kutozungumza na kutoskia huwa wanapitia madhila mengi na pia kushindwa kuelezea matatizo yao ya siri ili kupata msaada.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.