Tume ya kitaifa ya ardhi imetakiwa kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya kaunti ya Taita Taveta na Makaeni.
Haya ni kulinngana na kamishna wa tume ya uwiano na utangamano nchini NCIC Dorcas Kedogo ambaye amesema ikiwa utata huo utatatuliwa basi kutakuwa na uwazi wa mipaka kati ya kaunti hizo mbili sambamba na kuregesha amani kwa wenyeji ambao wanaishi maeneo hayo.
Akizungumzia mgogoro baina ya Wanyamapori na Wenyeji Kedogo amesema kwamba wizara ya fedha inasubiriwa kutoa muongozo wa malipo hayo baada ya sheria kupitishwa katika bunge la kitaifa huku wakaazi hao wakihimizwa kudumisha amani.
Tume ya NCIC imezuru kaunti ya Taita Taveta katika kujadiliana na makundi mbali mbali kuhusiana na namna ya kukabiliana na mizozo ikiwemo ya ardhi.