KAMISHNA WA KAUNTI YA KWALE JOSEPH KANYIRI AWATAKA WAZAZI NA WATAHINIWA WA KCSE KUTOHOFU LOLOTE

 

Kamishna wa kaunti ya Kwale Joseph Kanyiri amebainisha kuwa kamati inayohusika na maswala ya mitihani ya kitaifa kaunti hiyo imefanya mazungumzo na baraza la mitihani nchini KNEC kuhusu mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoibuka wakati ambapo mitihani ya KCSE inaendelea.

Kanyiri amesema changamoto kama zile za mafuriko zinazoshuhudiwa nyakati za mvua ni sharti zidhibitiwe ili zisihujumu shughuli nzima ya watahiniwa kufanya mitihani yao.

Kamishna huyo amesema kuwa tayari wametenga magari maalum ambayo yataweza kusafirisha mitihani kwenye vituo vya mitihani ambavyo huenda vikakumbwa na mafuriko.

Kanyiri amewashinikiza wazazi na watahiniwa kutohofia lolote kwani serikali kupitia kamati andalizi ya mitihani imejizatiti vilivyo kukabiliana na changamoto ibuka hasa wakati huu wa mitihani ya KCSE.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.