jumuiya ya kaunti za pwani yatakiwa kuingilia katiswala la bandari ya Mombasa

 

Seneta wa kaunti ya Mombasa, Mohamed Faki ameitaka serikali ya kitaifa kuhakikisha kuwa inaruhusu shughuli za mapokezi na upakuaji wa mizigo zifanyike kikamilifu katika bandari ya mombasa iwapo inajali maslahi wa wapwani.

KATIKA mahojiano ya kipekee na kituo cha Lulu fm Faki amesema kuwa kwa muda sasa wamepeleka hoja kuhusu bandari ya Mombasa katika bunge la seneti kupitia kamati ya usafiri na miundo msingi huku akiongeza kuwa watazidisha shinikizo zao ili kuona kwamba biashara za wapwani haziathiriki.

Faki ametoa wito kwa jumuiya ya kaunti za pwani kuingilia kati katika swala la bandari ya Mombasa badala ya kuwaachia wabunge pekee kwani mapato yakipungua katika bandari ya Mombasa yataathiri pakubwa katika utoaji huduma kwa kaunti zote 6 za pwani.

Kuhusiana na swala la utayari wa kaunti za pwani kuhusiana na kukabiliana na maambukizi ya virusi vya korona, Faki amesema kuwa kaunti za pwani zingali zinakumbwa na changamoto nyingi katika kufanikisha swala hilo huku akisema kuwa chimbuko la janga la covid 19 limedhihirisha kuwa serikali za kaunti zinapaswa kupiga hatua zaidi katika kuimarisha sekta ya afya.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.