Julie Oseko asema Visa vya ubakaji vinazidi kushuhudiwa katika jamii

 

Hakimu mkaazi katika mahakama ya Malindi kaunti ya Kilifi Julie Oseko amehoji kuwa licha ya janga la Corona kuathiri baadhi ya shughuli nchini bado mahakama ingali inaendeleza na shunguli zake kama kawaida.
Amesema kuwa kufuatia marufuku nyingi zilizo wekwa hasa wakati huu taifa linakumbwa na janga la Covid 19 kumekuwa na visa vingi ya ubakaji katika jamii ikilinganishwa na hapo awali kabla ya Corona.
Oseko amehoji kuwa visa vya ubakaji vimepewa kipaumbele katika mahakama hiyo na kuongeza kuwa tayari wamefanya vikao na washidau katika idara ya usalama na hata machifu walioko mashinani ili kubaini jinsi watakavyo saidia watoto wa kike ambao wamekuwa wakidhulumiwa.
Hata hivyo, amesema kuwa juhudi zimewekwa kuhakikisha kuwa visa vya ubakaji havichukui zaidi ya miezi sita huku akisema tayari zipo baadhi ya kesi ambazo wamefaulu kuziskiza na kutoa uamuzi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.