Joho asema wenyeji wa Mji wa Kale wanahujumu juhudi za kudhibiti Virusi vya Corona

 

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amesema kuwa wakaazi wa Mji wa Kale wanachangia katika kuhujumu juhudi za serikali za kudhibiti usambaaji wa virusi vya korona.
Joho amesema licha ya serikali kuimarisha jitihada za kutoa hamasa kwa wakaazi hao kujitokeza kwa wingi ili kupimwa kubaini iwapo wameambukizwa virusi vya Corona au la, bado wanasusia kushiriki katika zoezi hilo.
Huku hayo yakijiri afisa mkuu katika wizara ya biashara viwanda na utalii Aisha Abdi amesema kuwa serikali ya kaunti ya Mombasa inachukua wakati huu kulikarabati soko la Marikiti siku chache baada ya soko hilo kufungwa ili kuliboresha zaidi.
Aidha, amedokeza kuwa kufungwa kwa soko hilo ni mojawapo wa mbinu za kukabiliana na usambaaji wa virusi vya korona.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.