Jitihada za Leicester kwenye EPL top four baada ya kipigo cha 2-1 dhidi ya Villa

Meneja wa klabu ya Leicester City Brendan Rodgers anaamini kwamba kupoteza nusu fainali ya kombe la Carabao ni nafasi ya kuwapa wachezaji wake kuelekeza jitihada katika ligi ya ligi kuu ya Uingereza na kumaliza kwenye nne bora mbele ya Chelsea na Tottenham.

Mbweha hao waliruhusu kichapo cha 2-1 katika dakika za lala salama kwenye nusu fainali yao dhidi ya Aston Villa huku Trezeguet akifunga goli la ushindi na kuwahakikishia Villa safari ya Wembley kwa fainali dhidi ya Manchester City ama Manchester United.

Semi fainali ya pili ya mkondo wa pili itawakutanisha Manchester United na Manchester katika dimba la Etihad leo Jumatano saa tano kasorobo majira ya Afrika Mashariki.

Kwenye mkondo wa kwanza City waliwanyuka United magoli 3-1 wakiwa kwenye uwanja wa Old Trafford.

Rodgers aidha amesema kwamba vijana wake hawaavunjwa moyo kwa kupoteza mechi hiyo huku wakiwa na mechi dhidi ya Chelsea Jumamossi katika ligi kuu ya Uingereza.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.