JINSIA YA KIKE KATIKA USAJILI WA MAKURUTU KWENYE KIKOSI CHA IDARA YA POLISI YADAI KUBAGULIWA

Wanaharakati eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu wamelalamikia kukosa nafasi kwa wasichana katika zoezi la kuwasajili makurutu katika kikosi kitakachojiunga na idara ya polisi.

Wanaharakati hao wamegadhabishwa na swala la kuwa wasichana waliojitokeza kujiunga na idara ya polisi walitemwa nje na kudai kuwa waliagizwa waende wakaolewe.

Wamesema kuwa ingekuwa vyema iwapo idara hiyo ingeweka wazi kuwa wasichana hawataruhusiwa katika zoezi hilo badala ya kuwahangaisha katika siku ya usajili.

Aidha wamesema sio haki kwa watoto wa kike kunyimwa nafasi za ajira ilhali wana kila uwezo wa kupata nafasi hizo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.