Jamii yatakiwa kuwathamini walemavu

Jamii imetakiwa kuacha kuwatenga watu wanaoishi na ulemavu msimu huu ambapo taifa linakumbwa na janga la virusi vya corona.
Haya ni kulingana na Mwakilishi wa walemavu katika kaunti ya mombasa Ramla Said ambaye amesema tayari wameweka mikakati maalum ya kuwasaidia kupitia kuunda kituo maalum cha kuwasaidia walemavu cha Al-muqtadir Ability Centre huku wakifanikiwa kuwasaidia takribani walemavu 600.
Aidha amesema japo msimu huu wa janga la covid-19 umewapa changamoto walemavu wengi sasa wameamua kutoa hamasa kwa jamii inayoishi na ulemavu jinsi ya kujilinda dhidi ya virusi hivyo kama ilivyoagiza serikali kuu pamoja na idara ya afya.
Hata hivyo, ametoa wito kwa jamii kwa ujumla kufuata maagizo ya idara afya ili kujilinda dhidi ya ugonjwa huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.