Jamii yatakiwa kupiga ripoti kwa asasi za usalama wanaposhuku mtu anajihusisha na ugaidi

Naibu kamishna wa Kilifi kaskazini Josphat Mutisya amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuna usalama na Amani nchini.

Akizungumza katika kongamano la wanahabari wa kanda ya Pwani ambalo linaandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la KECOSCE, Mutisya amesema jamii inapaswa kufanya kazi kwa karibu na wazee wa Nyumba Kumi ili kukabiliana na watu ambao wanaolenga kutatiza Amani na usalama nchini.

Ametoa wito kwa jamii kuchukua hatua ya kupiga ripoti kwa asasi za usalama kila wanapomshuku mtu katika jamii ili hatua za haraka zichukuliwe dhidi ya washukiwa.

ata hivyo amehoji kwamba wazazi na jamii kwa jumla wanapaswa kuwa karibu na watoto wao kwa kuwaelekeza katika misingi iliyobora sambamba na kufuatilia mienendo yao ili kuwakinga dhidi ya vishawishi vya kujiunga na makundi ya kigaidi na imani potofu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.