VIPINDI

Amka Na Rafiki – Binti na Jahnoh

Binti Umazi na Jahnoh hukuletea kipindi Amka Na Rafiki kila asubuhi 6am-10am. Mziki wa kuhuisha, mada kemkem na uchambuzi wa magazeti utavipata ndaniya kipindi Amka Na Rafiki.

Changamka – Smartphone

Kila siku ya wiki kuanzia 10am - 2pm Smartphone hukuletea kipindi changamka kinachoangazia hoja na mada za kijamii. Ni kipindi pekee kinachotoa fursa ya msikilizaji kuitisha wimbo na kuchezewa.

Lulu Drive – DK

Lulu Drive ni kipindi kinachoendeshwa na DK kila siku ya wiki kuanzia saa tisa mchana hadi saa moja jioni saa za Afrika Mashariki.

Mkao – Kazungu Tumaini

Kipindi cha mkao kinakujia kila siku ya wiki kuanzia saa moja jioni hadi saa nne usiku. Kinaandazia maswala mbali mbali ikiwemo siasa, afya, ndoa, taarifa zinazojiri, pamoja na shuhuda za kujenga na kutia moyo.

Lulu Viwanjani – Sam Amani

Lulu viwanjani kinakuletea taarifa na zote za michezo kuanzia mashinani hadi katika soka la ughaibuni. Kipindi hiki kinakujia kila Jumamosi saa nane mchana hadi saa kumi.

Msuru Wa Mwamba – Sam Amani

Kila Jumamosi saa 5PM-6PM ni wasaa wa kipindi Msururu Wa Mwamba kinachoendeshwa na Sam Amani. Kinaangazia taarifa zilizogonga vichwa vya habari ndani ya wiki nzima.

Kama Vipi – Binti U

Kama Vipi inakujia kila Jumamosi kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa nne usiku kikiangazia maswala yanayomkumba kija wa karne ya leo.

Gospel Shangwe –  DK

Gospel Shangwe ni kipindi kinachoendeshwa na DK kila Jumapili kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne asubuhi saa za Afrika Mashariki.

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.