Muungano wa Judo Kenya waitaka serikali kulipa marupurupu ya wachezaji

Maafisa wa muungano wa Judo nchini Kenya wameonesha kughadhabishwa na serikali kupitia wizara ya michezo kufuatia kulimbikizwa kwa marupurupu pamoja na malipo ya tuzo ya wachezaji ya tangu mwaka wa 207.

Muungano huo umetangaza kwamba wachezaji wa vitengo mbalimbali wameingia kwenye mashindani tofauti pamoja na Africa Judo Championship yaliyoandaliwa Bujumbura, Burundi ila hawajalipwa marupurupu yao hadi kufikia sasa.

Akiongea wakati wa michuano ya Judo ya kaunti ya Kwale iliyoandaliwa Kwale wikendi, naibu rais wa muungao huo Duncan Chemirio amesema, wachezaji wa Judo kufikia sasa wamepoteza motisha wa kuendelea kucheza mchezo huo kufuatia kukosa kupewa marupurupu yao. 

Chimirio aliongeza kwamba mchezo huo umevutia wengi nchin kote huku vilabu 20 japo vilabu hivyo vimekosa motisha kwa kukosa fedha za kuendelea na mchezo huo. 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.