Mtengo ajitenga na madai ya miradi hewa Malindi

Aliyekuwa mbunge wa Malindi Willy Mtengo amepuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na wanaharakati wa kutetea haki za kibinadamu kuwa uongozi wake ulitekeleza miradi hewa chini ya mfuko wa hazina ya ustawishaji wa maeneo bunge yaani NG-CDF, akitaja kuwa potofu.

Kwenye mahojiano na meza yetu ya habari, Mtengo amesema hakuwa mamlakani katika muda ambao bajeti ya fedha imeibua utata kwa kusheheni miradi hewa akisema aliingia mamlakani na kuanza kuwahudumia wakazi wa malindi kutumia bajeti ya mwaka 2016/2017.

Amesema miradi yote ya kuanzia kuasisiwa kwa ugatuzi hadi mwaka 2016 ilitekelezwa na mtangulizi wake Balozi Dan Kazungu na kwamba kamati kamati ya afisi ya mbunge ya awamu hiyo inafaa kuwajibikia ufujwaji wa fedha hizo na wala sio wakati wa uongozi wake.

Wakati uo huo Mtengo ameyataka mashirika ya kijamii yanayofanya upelelezi wa matumizi ya fedha kufuata utaratibu ufaao akisema wakati huo wabunge hawakuwa na jukumu la kushuhulikia barabara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.