Mkufunzi wa Brighton atimuliwa siku chache baada ya kupoteza mechi dhidi ya Man City

Uongozi wa timu ya Brighton & Albion umemtimua kocha wake Chris Hughton siku moja baada ya kufungwa na Manchester City licha ya kuinusuru timu hiyo kushuka daraja msimu huu.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Tony Bloom kwenye taarifa yake ameeleza, Hughton amefanya kazi nzuri kwa miaka minne iliyopita hata hivyo wamelazimika kuachana nae.

Wakati huohuo, Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ambao ni mabingwa wa ligi kuu Uingereza msimu huu wa 2018/19 amewashukuru wapinzani wake klabu ya Liverpool kwa namna walivyokuwa wakimpa presha ya kupambana kwenye kila mechi.

Man City msimu huu wametwaa kombe wakiwa na tofauti ya alama moja pekee na Liverpool.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.