Mangi ashinikiza serikali za kuanti ya Tana River na Kilifi kusimamia mradi wa Galana -Kulalu

Viongozi kaunti ya Kilifi wanaendelea kuishinikiza serikali ya kitaifa kurejesha usimamizi wa mradi wa Kilimo wa galana kulalu kwa serikali za kaunti ya Kilifi na Tana River baada ya mradi huo kusambaratika.

Aliyekuwa mwakilishi wa wadi ya Bamba Daniel Mangi anasema serikali za kaunti hizo mbili zinauwezo wa kutosha wa kuendesha mradi huo ili kukabiliana na uhaba wa mara kwa mara wa chakula ambao umekuwa ukikumba kaunti hizo kutoka na vipindi virefu vya kiangazi.

Mangi anasema iwapo mradi huo utasimamiwa na serikali za kaunti basi swala la ukosefu wa chakula kaunti ya Kilifi na Tana River lingekabiliwa vilivyo kwani chakula kitakachozalishwa katika eneo hilo kingegawanywa moja kwa moja kwa wakazi wa kaunti hizo mbili.

Wakati uo huo ameishauri idara ya Kilimo kupitia kaunti ya Kilifi kupitia maafisa wake kutoa hamasa kwa wakulima aina ya mimea inayofanya vizuri katika eneo hili kabla ya kuanza kwa shuhuli za upanzi ili kuhakikishia mazao bora.

Itakumbukwa gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefa Kingi na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire walitaja ufisadi kama chanzo cha kusambaratika kwa mradi huo huku gavana Kingi akiitaka serikali kurejesha usimamizi wa mradi huo kwa serikali za kaunti ya Kilifi na Tana River.

Haya yanajiri huku wakazi wa kaunti hizo mbili wakikabiliwa na uhaba wa chakula cha kutosha kutoka na kiangazi kilichoshuhudiwa muda mrefu katika kaunti hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.