Polisi Kwale wawazuilia wanafunzi waliojaribu kuteketeza Bweni la Shule

Wanafunzi watano wa kidato cha pili katika shule ya upili ya Mwalufamba kaunti ya Kwale wanaendelea kuzuiliwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Kwale baada ya kujaribu kuteketeza bweni moja.

Wanafunzi hao wanadaiwa kwamba mwendo wa saa nane walikuwa wamepanga magodoro ishirini na tano ambayo tayari walikuwa wameyamwagia mafuta ya petrol kabla ya jaribio lao kutibuliwa na mlinzi wa shule hiyo.

Akithibitisha kisa hicho OCPD wa matuga Simon Gababa amewataka wanafunzi kusaka njia mbadala za kutatua matatizo yao badala ya kuchoma shule.

“Leo Asubuhi kama saa 2:30am wanafunzi hawa wamenaswa wakiwa katika pilkapilka za kuteketeza bweni moja na tukafika shuleni humo upesi na tukapata takribani magodoro ishirini na tano yamepangwa na kumwagiwa mafuta ya petroli tayari kuyachoma”, alisema Gababa

Gababa anasema tayari uchunguzi umeanzishwa huku wanafunzi hao wakitarajiwa kufikishwa mahakama Jumatatu wiki ijayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.