Mwanamke akatwakatwa kwa panga na mumewe Garashi kaunti ya Kilifi

Mwanamke mmoja anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi baada ya kukatwakatwa kwa panga na mume wake katika kijiji cha Bora Koromi wadi ya Garashi kaunti ndogo ya Magarini.

Kulingana na mwakilishi wa wadi hiyo Peter Ziro akizungumza katika hospitali hiyo, ni kwamba Christine Sidi alitendewa kitendo hicho na mumewe Kahindi Mwambire usiku wa kuamkia leo. Amewataka maafisa wa polisi kuhakikisha wanamtia mbarano mshukiwa huyo na kumfungulia mashtaka mara moja.

“Ni bwana mmoja ambaye anatuhumiwa kukatakata mapangwa mkewe kufuatia ugomvi waliokuwa nao na kama kiongozi nalaani vikali kitendo hiki na huyu bwana anafaa kuchukuliwa hatua za kisheria mapema iwezekanavyo,” amesema Peter Ziro.

Aidha sidi amekiri kuwapo kwa ugomvi baina yake na mumewake akimshtumu kukosa kujukumikia ipasavyo katika malezi ya watoto wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.