Huenda ukame ukaendelea kushuhudiwa Tana River

Serikali imesema hali ya ukame katika kaunti ya Tana River itaendelea kushuhudiwa na kwamba huenda ikafikia kiwango cha hatari zaidi, iwapo mvua haitashuhudiwa kama inavyotarajiwa.

Kamishna wa kaunti hiyo Oningoi Olesosio amesema ripoti kutoka kwa idara ya kukabili ukame imesema kiwango cha ukame kimezindi kupanda ikilinganishwa na mvua inayonyesha eneo hilo.

Licha ya sehemu kadhaa za Tana Delta kushuhudiwa mvua, bado sehemu nyingi katika eneo hilo zinakabiliwa na ukame.

Tayari jamii ya wafugaji katika kaunti hiyo imeanza kuhamia maeneo yanayoshuhudiwa mvua huku ikifasiriwa kwamba huenda htua hiyo ikaibua migogoro baina ya jamii husika.

“Tunahofia kwamba huenda kukazuka migogoro kwa sababu upande huo ambako kunashuhudiwa mvua wafugaji wameanza kuhamia huko,. Taarifa kutoka kitengo cha ukame nchini kimeonyesha kwamba hali sio nzuri ikiwa hakutashuhudiwa mvua, Tayari wafugaji wameanza mbinu ya kuhamahama”,alisem Olesossio

Haya yanajiri huku serikali kupitia shirika la msalaba mwekudu likiendeleza mpango wa ujenzi wa makazi kwa familia zilizoathirika na mafuriko mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.