Watu 49 wauawa na 20 kujeruhiwa katika shambulizi la misikiti, New Zealand

Serikali ya New Zealand kupia waziri mkuu, Jacinda Ardern, imesema watu 49 wameuawa na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya kuzuka mashambulio katika misikiti miwili katika mji wa Christchurch huko New Zealand.

Ardern amelitaja shambulio hilo kuwa lililotanda ‘kiza kikubwa’ siku ya leo nchini humo. Wanaume watatu na mwanamke mmoja wamekamatwa na Kamishna wa Polisi, Mike Bush, na kuonya kwamba huenda washukiwa zaidi wapo.

Inaarifiwa kwamba washambuliaji hao hawakuwa kwenye orodha ya magaidi wanaosakwa lakini ni wazi kwamba wana itikadi kali.

Aidha waziri mkuu wa Australia, Scott Morrison, amesema miongoni mwa waliokamatwa ni raia wa Australia.

Walioshuhudia mkasa huo wameviambia vyombo vya habari kwamba walilazimika kutoroka kuokoa maisha yao na waliona watu walioanguka chini na wanaovuja damu nje ya Msikiti wa Al Noor.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.