Shalke 04 yamuachisha kazi kocha baada ya kipigo cha Mancity

Klabu ya Schalke 04 imemfuta kazi mkufunzi Domenico Tedesco kufuatia kipigo cha mabao saba (7) kwa nunge mikononi mwa Klabu ya Mancity kwenye hatua ya mwisho ya kumi na sita (16) ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Aliyekuwa mkurugenzi wa klabu hiyo Huub Stevens pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati Mike Buskens wanatarajiwa kuchukua nafasi hiyo ya ukufunzi kabla ya mchuano baina ya klabu hiyo na RB Leipzig kwenye ligi ya Bundesliga Jumamosi ya tarehe 16.

Schalke imepoteza michezo mitano ya hapo awali na wako hatua tatu tu juu ya eneo hatari la kutoka kwenye ligi.

Tedesco mwenye umri wa miaka 33 aliajiriwa na klabu hiyo mnamo Julai mwaka juzi 2017 na ameweza kusimamia michuano 75 katika klabu hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.