Polisi Malindi wanawazuilia maafisa 6 wa KWS

Maafisa wa polisi mjini Malindi wanawazuilia maafisa sita wa shirika la huduma kwa wanyamapori wanaohudumu katika mbunga ya wanayamapori ya Tsavo mashariki kwa madai ya kumpa kichapo mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka hamsini.

Afisa mkuu wa idara ya upelelezi kaunti ya Tana River Wyclif Sifuna anasema sita hao wanadaiwa kumuua mwanamume huyo aliyekuwa akichunga mifugo wake akiandamana na wanawe watatu.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba watoto hao walikamatwa na kufungwa katika jela za watoto mjini Voi baada ya kushuhudia babayao akipigwa risasi kabla ya kudaiwa kutupwa ndani yam to galena.

Ni tukio ambalo linadaiwa kutekelezwa mnamo tarehe ishirini na nne mwezi disemba mwaka jana na kufichuliwa na watoto wa mwendazake pindi tu walipoachiliwa huru.

Tukio hili linajiri huku mashirika mbalimbali ya kutetea haki za kibinadamu katika kanda ya pwani yakiendelea kuwashinikiza maafisa katika idara ya polisi kuzingatia sheria wanapokabiliana na mshukiwa wa uhalifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.