Kocha wa Kakamega Homeboyz aeleza sababu ya kufungwa na Gor Mahia

Kocha mkuu wa Kakamega Homeboyz Nicholas Muyoti amesema kukosa umakini ndio sababu kuu ya kufungwa magoli mawili kwa moja na klabu ya Gor mahia hiyo jana Alhamisi katika ligi kuu nchini KPL.

Homeboyz waliongoza ila awamu ya pili ya mchezo Gor Mahia ikajipatia magoli mawili na kulingana na Muyoti ni kuwa magoli hayo ya haraka yaliwachanganya wachezaji na kuwafanya wakose kuwa makini

Muyoti aidha amekubali kwamba hawakujitengenezea nafasi katika mchezo tofauti na mazoea yao na kuahidi kufanya bidii pamoja na kurekebisha makosa wanapokutana na Mathare United jumapili ya tarehe 17 mwezi Machi.

Kwa sasa klabu ya Kakamega Homeboyz inashikilia nafasi ya 9 wakiwa na alama 21; wamepoteza michuano miwili, kushinda miwili na kutoka sare mara moja ndani ya michuano mitano ya hivi punde.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.