Joho ashinikizwa kutatua mvutano katika serikali yake

Shinikizo zinazidi kutolewa kwa gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho kuandaa mazungumzo na washakdau katika serikali yake ili kuhakikisha kwamba kuna uadilifu katika utendakazi wao kwa mwananchi.

Mwanaharakati wa maswala ya kisiasa kaunti ya Mombasa Ben Oluoch anasema kuna haja ya gavana Joho kutoa muelekea kwa wawakilishi wa wadi katika bunge la kaunti hiyo pamoja na mawaziri ili kuzima malumbano baina ya asasi hizo mbili muhimu.

Wakati huo huo Oluoch amemtaka waziri wa mazingira katika kaunti hiyo kuweka mipango madhubuti ya kusafisha mitaro ya maji taka kabla mvua kuanza.

Mnamo Jumanne wiki hii wakazi walianzisha mchakato wa kukusanya sahihi zitakazowezesha kuvunjiliwa mbali kwa bunge la kaunti ya Mombasa chini ya vuguvugu la ‘fagia bunge’.

Wakiongozwa na katibu wa vuguvugu hilo, Mgandi Kalinga wanapania kukusanya sahihi laki mbili ambazo wataziwasilisha kwa raisi ili bunge hilo livunjwe.

Wamedai kuwa wawakilishi wadi wanaendelea kuzembea na kutumia fedha za miradi mbali mbali kwa manufaa yao binafsi bila kujali masuala ya wananchi waliowachagua.

Kalinga amesema kuna ushahidi wa kutosha kuwasilisha mbele ya mamlaka husika kwa ajili ya kuvunjiliwa mbali bunge hilo na wananchi kurudi debeni ili kuchagua viongozi wengine watendakazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.