Fainali ya kombe la dunia kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 20 kuhudhuriwa na mashabiki wengi zaidi

Shirikisho la soka duniani FIFA, limesema kuelekea fainali ya kombe la dunia kwa vijana wasiozidi miaka 20, tayari tiketi zaidi ya 100,000 zimeuzwa.

Fainali hiyo itafanyika nchini Poland kati ya tarehe 23 mwezi Mei hadi Juni 15 mwaka 2019. Ripoti zinaonesha kuwa mashabiki wengi wamenunua tiketi za kushuhudia mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Poland na Colombia itakayochezwa katika uwanja wa Widzewa mjini Lodz.

Wenyeji Poland wamepangwa katika kundi la A pamoja na Colombia, Tahiti na Senegal.

Kundi B: Mexico, Italia, Japan na Ecuador.

Kundi C: Honduras, New Zealand, Uruguay, Norway

Kundi D: Qatar, Nigeria, Ukraine na Marekani

Kundi E: Pana, Mali, Ufaransa, Saudi Arabia

Kundi F: Ureno, Korea Kusini, Argentina, Afrika Kusini

Mataifa 24 yatashiriki katika fainali hizo za 22 na bara la Afrika litawakilishwa na Senegal, Nigeria, Afrika Kusini na Mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.