Arsenal yatinga hatua ya robo fainali ligi ya mabingwa Ulaya

Licha ya kuwa na kibarua kikubwa jana, Arsenal imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Rennes katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Katika mechi ya awali, Arsenal walipoteza kwa mabao 3-1 wiki iliyopita dhidi ya club ya Rennes inayoaminika kuwa ya kawaida kutoka ligi ya Ufaransa.

Kwingineko klabu ya Chelsea maarufu kama the blues imefanya mauaji kwa kuipiga mabao 5-0 Dynamo Kyiv. Nao Benfica imeshinda kwa goli 3-0 dhidi ya Dinamo Zagreb, FC Krasnodar imeilazimisha sare ya 1-1 Valencia, nayo Napoli imekubali kipigo cha 3-1 toka kwa Salzburg, huku Inter Milan ikifungwa goli 1-0 na Eintracht Frankfurt. Slavia Prague wao wameibamiza Sevilla bao 4-3 nao Villarreal ikiibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Zenith St. Petersburg.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.