Serikali ya kaunti yatakiwa kuboresha makazi ya wazee

Wazee wa Kaya za Mijikenda kaunti ya Kilifi wameitaka serikali ya kaunti hiyo kupitia kwa idara ya utamaduni kuboresha makazi ya wazee yaliyoko huko Mrima wa Ndege kaunti ndogo ya Ganze ili kuhifadhi wazee ambao wamenusurika kifo kutokana na tuhma za uchawi.

Akizungumza na wanahabari mwenyekiti wa wazee wa kimijikenda katika kaunti hiyo Stanly Kenga amesema badala ya hifadhi hiyo kutumika kama mahala pa kuwaokoa wazee waliokataliwa na familia zao kwa tuhuma za uchawi itakuwa bora zaidi iwapo wazee wengine pia watawezwa kuhifadhiwa ili kuepukana na ugumu wa maisha.

Stanly ameeleza kuwa makazi hayo kwa sasa yako katika hali duni licha ya viongozi mbalimbali kuahidi kuboresha makazi hayo.

Kwa upande wake afisa mkuu wa idara ya michezo, jinsia na utamaduni katika kaunti hiyo Bi. Mwenda Karisa ni kuwa hifadhi hiyo pia itaweza kumaliza dhana ya uchawi miongoni mwa wazee endapo itaboreshwa. 

Hata hivyo Mwenda ameahidi kupanga mikakakti ili kuweza kuona ni vipi suala hilo litaweza kukabiliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.