Mwambire amtaka gavana kuingilia kati mzozo wa wafugaji Bamba

Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire sasa anamtaka gavana wa Kaunti hio Amason Jeffa Kingi kuanza mchakato unaolenga kumaliza mizozo baina ya wafugaji na wenyeji wa maeneo ya Mitangani ambao imekuwa ikishuhudiwa mara kwa mara.

Akiongea huko Ganze Mwambire amesema ni kupitia hatua hio ndio itakayotoa mwelekeo mwafaka na hata kumaliza kabisa mitafaruku ambayo imekua ikishuhudiwa baina ya jamii hizo.

Mwambire hata hivyo amesistiza kwamba serikali ya Kaunti hio ndio inapaswa kutatua swala hilo ikizingatiwa wizara ya kilimo iligatuliwa.

Ametaja hatua ya wawekezaji kupelekwa katika maeneo hayo kuchagia katika mzozo huo ambao wenyeji wamekuwa wakikinzana vikali na maamuzi hayo licha ya yeye mwenye kuwasilisha malalamishi hayo mbele ya asasi husika.

“Kuna matatizo makubwa kwa sababu kuna wawekezaji ambao waliletwa hapa bila kufuata utaratibu unaostahili. Na tuliongea na asasi husika na liko katika serikali ya ugatuzi kwa kuwa hakuna mtu anayeweza kuleta mifugo kutoka sehemu nyengine hadi hapa Kilifi pasipo na idara ya ufugaji kufahamishwa. Kwa sababu ukiangalia mwaka juzi mifugo wengi waliletwa hapa na kilichofuata ni chakula cha mifugo wetu kutumiwa chote”, alisema Mwambire.

Itakumbukwa wenyeji wa maeneo ya Mitangani huko Bamba walikuwa tayari wameanza kuchoma misitu na nyasi kama njia moja wapo ya kuwafurusha wafugaji hao kilazima ambapo Zaidi ya ekari saba za misitu zilikua zimechomwa,huku wakidai maafisa wa utawala katika sehemu hio ndio wanalemeza juhudi za kupatikana kwa suluhu la kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.