IMEBAINIKA KWAMBA IDADI KUBWA YA VIJANA WANAOTUMIA MIHADARATI IMEONGEZEKA KANDA PWANI

Idadi kubwa ya vijana kanda ya pwani wanaotumia dawa za kulevya imetajwa kuongezeka.

Akizungumza na meza yetu ya habari chifu mkuu wa kata ndogo ya Voi ya kaunti ya Taita Taveta, Abel Mwangemi amehoji kuwa swala la jamii kutoshirikiana na serikali katika vita hivi dhidi ya ulanguzi wa mihadarati ni moja wapo ya mambo ambayo yamechangia katika ongezeko la idadi hiyo.

Aidha Chifu huyo amesema kuwa licha ya juhudi zao za kuwashika waotengeneza pombe yapo baadhi ya makundi ambayo hulipa faini ya wale wanaokamatwa na maafisa wa polisi hali ambayo imekuwa ikilemaza oparesheni.

Mwangemi ameiomba serikali ya kaunti hiyo na serikali kuu kushirikiana pamoja ili kupata njia mwafaka ya kukabiliana na swala la matumizi wa dawa za kulevya katika kaunti hiyo kwani vijana wengi tayari wamekuwa waraibu wa dawa hizo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.