Ighalo aipelekea Man United robo fainali kombe la FA

Klabu ya Man United usiku wa kuamkia leo ilikuwa ugenini kucheza game yake ya 16 bora ya FA Cup dhidi ya Derby County ikiwa ndio mbio za kuwania kutinga robo fainali.

Mchezo huo wa Man United ulikuwa unawakutanisha na mchezaji wao wa zamani Wayne Rooney aliyeishia kuona timu yake ya Derby ikipoteza kwa magoli 3.0.

Hata hivyo baada ya Luke Shaw kufunga goli la uongozi dakika ya 33, Jude Ighalo ambaye anatajwa kama ingizo jipya akafunga magoli mawili dakika ya 41 na 70 na kuitendea haki nafasi hiyo ikiwa yupo hapo kwa mkopo, Man United sasa inatinga robo fainali na watacheza dhid ya wababe wa Spurs club ya Norwich City.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.