Idara ya usalama Kilifi inamzuilia jamaa ambaye amemkatakata mkewe

Kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi, James Mugera amesema wanamzuilia mwanamume mmoja kwa jina Festus Baya Maitha mwenye umri wa makamu kwa kosa la kumuua kwa kumkatakata mapanga mkewe katika eneo la Boyani eneo bunge la Ganze.
Kwa mujibu wa Mugera ni kwamba jamaa huyo alichukua hatua ya kumkatakata mkewe kwa jina Claris Amina kwa madai ya kuchepuka katika ndoa.
Hata hivyo, kufuatia kisa hicho Kamanda huyo wa polisi amewahimiza wanandoa wotre kutochukua sheria mkononi kila wanapokumbwa na misukosuko ya ndoa na badala yake kutafuta ushauri nasaha kutoka kwa washauri ili kuepuka visa hivyo vya mauaji.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.