IDARA YA KILIMO KAUNTI YA KWALE KUKABILIANA NA UVAMIZI WA WADUDU WANAOHARIBU MIMEA

Mkurugenzi katika idara ya kilimo kaunti ya Kwale, Safari Ziro amesema kuwa idara hiyo imejipanga kuona kwamba inakabiliana na uvamizi wa wadudu wanaoharibu mimea hasa wakati wa upanzi.

Ziro amesema kuwa wakati huu ambapo mvua ya masika imeanza rasmi kuna uwezekano wa kushuhudiwa kwa uvamizi wa wadudu katika mimea mbalimbali ikiwemo mahindi.

Mkurugenzi huyo amekariri kuwa tayari wamesambaza dawa kwa wakulima kwa minajli ya kudhibiti wadudu hao.

Ziro amewashauri wakulima kunyunyiza dawa hizo kwenye mimea yao wakizingatia muda mwafaka kwani ni sharti mimea hiyo imee kwa muda kabla ya kunyunyiziwa dawa hizo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.