Idadi ya walioambukizwa corona nchini yafikia 303

Serikali ya kitaifa kupitia wizara ya afya imepiga marufuku kuingia na kutoka katika kaunti ya Mandera kufuatia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona katika kaunti hiyo.
Kwa mujibu wa waziri wa afya nchini,Mutahi Kagwe serikali imechukua hatua hiyo kwa kile ilichosema kuwa kaunti ya Mandera ipo karibu na mataifa yaliyo na wakimbizi ikiwemo taifa la Ethiopia na Somalia.
Haya yanajiri huku waziri Kagwe akifungamana na kauli ya rais Uhuru Kenyatta na kutoa onyo kali kwa wale wote wanaotoroka katika sehemu za karantini akisema kuwa wanachangia kuhatarisha maisha ya wakenya wengine jambo litakalowapelekea kukabiliwa vikali kisheria.
Waziri Kagwe amezidi kuwasihi wakenya kufuata maagizo yanayotolewa na serikali huku akitangaza kuwa watu wengine 7 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya korona nchini jumla ya watu walioathirika ikifikia 303.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.