HUENDA WANAFUNZI WAKAKOSA KUTIMIZA SHERIA YA KUKAA UMBALI WA MITA MOJA SHULENI

Waziri wa elimu nchini Profesa George Magoha amesema kuwa huenda taasisi za elimu nchini zika kosa kutimiza sheria ya kukaa umbali wa mita moja unusu.

Akizungumza na wanahabari Magoha amesema kuwa kufuatia hatua ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi katika baadhi ya shule huenda walimu katika taasisi hizo wakalazimika kubuni mbinu mbadala itakayo afikia agizo hilo la kudhibiti maambukizi ya Covid19 shuleni.

Waziri huyo ameongeza kuwa serikali ya kitaifa ikishirikiana na wizara zingine nchini zimepokea idadi ya barakoa milioni saba zitakazo gawiwa wanafunzi wanatoka katika familia zenye uhutaji.

Hata hivyo Waziri Magoha amesisitiza kuwa sharti wanafunzi wote katika shule za serikali na hata zakibinafsi wakubaliwe kurudi shule licha ya wao kutokuwa na karo huku akiwatahadharisha wale watakao kiuka agizo hili kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.