Huenda miradi ya maendeleo ikasitishwa Taita Taveta

 

Waziri wa fedha na maswala ya kiuchumi kaunti ya Taita Taveta Andrew Kubo amesema serikali ya kaunti hiyo huenda ikasitisha miradi yote ambayo ilikuwa ikitekelezwa katika kaunti hiyo kwa kipindi cha miezi mitano ijayo kama njia moja ya kuiwezesha serikali kulipa madeni yake.
Haya yanajiri baada ya kubainika wazi kwamba wanakandarasi mbali mbali wamekuwa wakidai kaunti hiyo kima cha shilingi milioni 652 katika miradi yote ambayo ilikuwa imeorodheshwa kutekelezwa mwaka wa 2019 / 2020.
Hata hivyo amesema licha ya kunti hiyo kukumbwa na changamoto ni sharti wanakandarasi kulipwa madeni yao baada ya kupitishwa kwa makadirio ya fedha za ziada.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.