huduma za upasuaji na kliniki za wagonjwa wenye kisukari na wale wenye shinikizo la damu zasitishwa kwa muda kwenye hospitali ya rufaa kaunti ya Kilifi mjini Kilifi

Mkuu wa hospitali ya rufaa kaunti ya Kilifi mjini Kilifi Dkt. Eddy Nzomo amesema hospitali hiyo itatoa huduma za dharura pekee ili kuzuia watu kusongamana ili kuzuia kuwaweka katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Nzomo amehoji kwamba huduma hizo za dharura zinajumuisha chanjo za watoto na kliniki za kina mama wajawazito na kuongeza hatua hiyo inalenga kuwakinga wakaazi sambamba na wahudumu wa afya dhidi ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Aidha Nzomo amesema kuwa ni marufuku kwa weneyji kuwatembelea wagonjwa huku akiongeza kuwa huduma za upasuaji na kliniki za wagonjwa wenye kisukari na wale wenye shinikizo la damu pia zimesitishwa kwa muda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.