Hat-trick ya Sterling yamfanya Gurdiola kumuitwa mchezaji mwenye kipaji maalum

Pep Guardiola ammmiminia sifa kedekede Raheem Sterling na kumuita kama mtu mwenye kipaji maalumu baada ya jana kuingia nusu ya pili na kufunga hat-trick ndani ya dakika 11, ambapo ameisaidia Manchester City kuivuruga vibaya Atalanta kwa kuondoka na ushindi wa magoli 5-1 na kuimarisha mwanzo wao mzuri kwa 100% kwenye Ligi ya Mabingwa Kundi C.

Sterling ni mfungaji anayeongoza wa Manchester City akiwa na magoli 12 aliyoyapata kwenye michezo 13 katika mashindano yote ya msimu huu na magoli aliyoyapata kwenye mchezo huu yamethibitisha uwezo wake mkubwa aliokuwa nao.

Hata hivyo Guardiola anahisi Sterling ana uwezo mkubwa zaidi mbali na kufunga magoli tu.

Amesema mwili wake uko imara, ana nguvu, na siku moja baada ya kucheza mechi anaweza kucheza mechi nyingine bila wasiwasi wowote.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.