Gunners mbioni kumuuza Auba na Lacazette

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amesema atalazimika kuwauza Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette katika usajili wa majira ya kiangazi.

Arteta amesema atachukua hatua hiyo kama Arsenal itashindwa kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kauli ya Arteta imekuja baada ya Arsenal kutolewa kwenye mashindano ya Kombe la Ulaya kwa kufungwa na Olympiakos. Wengine wanaotajwa kuuzwa ni Granix Xhaka na Shkodran Mustafi.

Hadi kufikia sasa klabu ya Arsenal ambayo ina alama 37 inasimama katika nafasi ya 10 ikiwa imecheza mechi 27. Imetoka sare mara 13 imepoteza mechi 6 na kushinda mechi nane.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.