GAVANA WA MOMBASA AWATAKA WAKAAZI WA MSAMBWENI KUPIMGIA KURA OMAR BOGA WA ODM

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amewarai wakazi wa Msambweni kumpigia kura Omar Boga wa chama cha ODM kwenye uchaguzi ambao umeratibiwa kufanyika tarehe 15 mwezi wa Desemba mwaka huu.

Joho amehoji kuwa wakaazi wa Msambweni wana matatizo mengi yatakayosuluhiswa na kiongozi anayeweka maslahi ya wananchi mbele, na kwamba atakapoingia bungeni atawajibikia maswala ya utalii na uvuvi kwa ushirikiano na serikali.

Aidha, mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya Kwale Hassan Mwanyoha amesema kuwa wanafanya kampeni za mashinani kutoka nyumba hadi nyumba kutokana kwa kuzingatia masharti ya wizara ya afya kufuatia janga la virusi vya Corona nchini.
Boga atamenyana na Feisal Abdalla anayewania kiti hicho kama mgombea huru anayepigiwa upato na naibu rais William Ruto.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.