Gavana Samboja awataka washikadau wa elimu kukabiliana vilivyo dhidi ya wizi wa mitihani ya kitaifa

Gavana wa kaunti ya Taita-Taveta, Granton Samboja amewataka washikadau wa elimu katika kaunti hiyo wakishirikiana na idara husika kuweka mikakati ili kukabiliana na wizi wa mitihani.

Samboja amesema mitihani hiyo ni muhimu kwani itasaidia kujua uwezo wa wanafunzi huku akiwahimiza wazazi kushirikiana na watahiniwa katika kuweka mazingira mazuri pindi mitihani hii itakapoanza.

Gavana huyo pia amewasihi wazazi kuwapunguzia majukumu watahiniwa hasa wale wanaosoma shule za kutwa ili wakapate muda mzuri wa kujitayarisha kwa ajili ya mitihani yao.

Kauli ya gavana inajiri huku wizara ya elimu nchini hakikisho kuwa mikakati imewekwa ili kukabiliana na visa vya udanganyifu.
Mtihani wa kitaifa kwa shule za upili KCSE umeratibiwa kuanza tarehe 4 mwezi ujao na kutamatika tarehe 27 mwezi wa kumi na moja kote nchini Kenya.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.